Kwa mujibu wa idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, uongozi wa «Azakhana» na Husseiniya nchini Bahrain umelaani hatua iliyotolewa na taasisi rasmi inayowataka makhatibu, wazungumzaji na waombolezaji wanaoshiriki katika maadhimisho ya kidini kupata vibali vya awali.
Uongozi wa Azakhana na Husseiniya ulitangaza katika taarifa ya pamoja kwamba: Hatua zinazofuatana ambazo zimeathiri masuala ya kidini katika kipindi cha hivi karibuni, zikiwemo vikwazo vilivyowekwa katika kuendesha shughuli za maombolezo ya Muharram, pamoja na uamuzi wa kuunganisha taratibu za usimamizi wa Husseiniya na mali za wakfu, na sasa hatua hii mpya, zinaunda mlolongo na mwendelezo ambao hauwezi kutazamwa nje ya muktadha wake; kwani kwa ujumla wake, zinafichua kulengwa kwa utaratibu wa uhuru wa kutekeleza ibada za kidini zinazowahusu Mashia na kuingiliwa kwa upekee na uhuru wa madhehebu ya Jaafari.
Walisema kwa msisitizo: Hatua hizi zinakinzana na kifungu cha «22» cha Katiba ya Bahrain; kifungu ambacho kinasema: «Uhuru wa dhamiri ni kamili, na serikali inahakikisha kuheshimiwa kwa maeneo ya ibada, uhuru wa kutekeleza ibada za dini, maandamano na mikusanyiko ya kidini kwa mujibu wa mila na desturi zinazotumika nchini.»
Waliongeza: Hatua hii ni uingiliaji wa wazi katika masuala ya kidini na kuweka mamlaka juu ya mimbari na majlisi za Husseini. Aidha, walisisitiza kushikilia haki ya Azakhana, Husseiniya na taasisi za kidini kutekeleza wajibu wao na kuendesha ibada na maadhimisho yao kwa mujibu wa hukumu na kanuni za Sheria, mbali na aina yoyote ya utawala wa mabavu au uingiliaji.
Maoni yako